26 Septemba 2012 - 20:30

Vyombo vya habari vyatangaza kuwa Rais wa Misri aishambulia Israeli kama alivoishambulia Rais (Amad Najadi) wa Iran

Siku ilopita Rais Ahmadi Najadi wa Iran katika hutuba yake katika kikao cha jumuai ya umoja wa mataifa nchini Marekani kwa mara nyengine tena ameushambulia utawala wa kidhalimu wa Israeli nakuseama kuwa utawala huo umewekwa kwalengo la kufanya ubeberu duniani, naye aliongeza kusema kuwa nguvu za kimarekani pia ni msingi mkubwa wa matatizo yote duniani, nakuitaka dunia kutawaliwa na mfumo mpya.Baada ya hutuba ya Rais wa Iran alipanda jukwaani Rais Muhammad Mursiy  wa Misri ikiwa ni mara  yake yakwanza kuzungumza katika jumuia hiyo, Rais huyo pia aliiponda kanuni ya kimarekani ya uhuru wa kuzungumza ambayo inatoa ruhusa ya kutukanwa manabii wa Mungu ikiwemo kutengeneza filam inayo mtusi mtukufu mtume wa uislamu, naye pia alimuunga mkoni Rais wa Iran katika kuishambulia Israeli.